MAMA SHUPAVU, MAMA MPENDWA, MAMA MWALIMU

Naandika haya kwa machungu usiku wa leo nikifikiri kuwa iligharimu changamoto kutoka kwa mwanafunzi mwenza aliyedhani kuwa siwezi kuandika kwa lugha ya Kiswahili, ndipo nikaamua kufanya hili. Nimeandika kuhusu mengi katika maisha yangu tangu niufungue ukurasa huu lakini la kushangaza ni kuwa sijaandika kumhusu mamangu mpendwa hata wakati mmoja. Ama kweli ukishayazoea mengi mazuri ambayo mtu amekutendea, huenda yakabadilika na kukufanania kama haki na ukasahau kuwa na shukrani.

Lakini kuambatana na filosofia yangu katika maisha, sitayatilia mkazo mambo haya hasi bali nitatumia changamoto hii kutoka kwa mwenzangu huyu kuchambua yale chanya maishani kuhusiana na mama mpenzi.

Ama kweli ingekuwa ni uwongo kama ningedai kuwa ningeweza kuyaweka kwa maandishi yote ambayo mama amenitendea na kunifunza tangu aliponizaa hadi hapa nilipofika. Na kama jinsi msanii Tupac alivyoimba, kweli siwezi nikamlipa mama kwa yale aliyonitendea, lakini natumai kuwa matendo yangu yataonyesha shukran kwa hayo yote. Ni mengi ambayo ningeyasema kumhusu mama, lakini leo nitaongea kumhusu mwanamke shupavu ninayemjua na ambaye nimeishi naye kwa miaka ishirini na mitatu.

Haijapita muda mrefu, yapata miezi mitatu hivi iliyopita, mama alimpoteza babake na wakati huo nilikuwa mbali kidogo kwani nilikuwa nafanya tarajali yangu na nilikuwa ofisini baba aliponipigia simu kunifahamisha kuwa babu alikuwa amefariki. Ilinichukuwa takriban masaa matatu hivi kabla ya kupata ujasiri na kumpigia mama simu ili nipate kumjulia hali. Lakustaajabisha ni kuwa hata nilipompigia simu sauti yake haikuwa na ishara ya machungu na maumivu kama nilivyokuwa nimeogopa hapo awali. Mama alinieleza kuwa nia yake ilikuwa ni kusherehekea maisha ya babu, jambo ambalo lilinitia moyo sana.

Kadri siku zilivyozidi kusonga na siku ya mazishi ya babu kukaribia kuna mengi ambayo niliyaona na kujifunza katuko kwa mama. Na wakati huu wote mama alikuwa kama nguzo yangu na alinitia moyo sana kwa nguvu alizokuwa nazo licha ya kufiwa. Wakiti wote licha ya majonzi yaliyokuwepo hakubadilika na kuwacha kuwa mama niliyemjua tangu utotoni. Alituonyesha mapenzi kama wanawe na alihakikisha kuwa tulipata yote tuliyoyahitaji na hata tulipoenda nyumbani licha ya kuwa na umati mkubwa alihakikisha kuwa yote yalikuwa shwari kwa wanawe. Aliondoa bughudha zozote zile ambazo huhusishwa na sherehe za mazishi katika jamii yetu ya Waluo.

Wakati mwingi tumekuwa katika hali sawa na hii ya mama. Wakati ambapo maisha huwa ni magumu na yakajawa na majonzi. Wengi wetu husahau yote maishani na kutilia maanani mambo haya hasi. Wakati mwingine kuyafanya maisha kusimama na hata kuwasahau wale ambao hutupa nguvu katika maisha yetu na shuguli zetu za kila siku. Majonzi ni awamu tu katika maisha na kama zingine zote hupita. Ndugu yangu mdogo huniambia mara kwa mara ninapoyalalamikia maisha kwamba nilipozaliwa hakuna yeyote aliyenipa uhakika kwamba maisha yangekuwa rahisi. Kwa hayo nimeamua kuwa nitaufuata mwelekeo wa mama, na kuyakubali maisha jinsi yalivo wakati wa majonzi na wakati wa raha. Na kwa yote nitatahakikisha kuwa nimekuwa mtu bora kwa wote nitakao ingiliana nao. Sitabadilika kwa wakati wowote na kusingizia matukio. Asante kwa mafunzo haya mama, daima nitakupenda.      

Advertisements

3 thoughts on “MAMA SHUPAVU, MAMA MPENDWA, MAMA MWALIMU

  1. vivian says:

    ash is soo in mashaka.was was tht attachment name again? I feel challenged.kazi nzuri hapo.

  2. vivian says:

    ash is soo in mashaka.wat was tht attachment name again? I feel challenged.kazi nzuri hapo.

  3. Mak'Omondi says:

    There comes my dear Viv, always watching my back. Ash alinidharau bila kujua Kiswahili ndilo somo nililolipenda kabisa nilipokuwa shule ya upili. Nina uhakika unauliza neno TARAJALI. Thanx wifey.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s